Campus News Entertainment Music Music

SKY 254 KUNDI LINALOTESA KIMUZIKI NCHINI KENYA

Pizzah Mwitu
Written by Pizzah Mwitu
Spread the love

SKY 254 ni bendi la muziki linalotesa sana nchini Kenya. Kundi hili linajumuisha wasanii watatu walio na vipaji na ambao hawabahatishi na kile wanachokifanya na wanajituma asilimia Mia. Watatu hao ni Jaymah Hapa, Stamusic na DJ blackieblack ambao ni wanafunzi wa chuo kikuu cha Laikipia. Grupu hii inaongozwa na Msanii Jaymah Hapa ambaye alikuwa akifanya Kazi kivyake kabla ya kujiunga na wenzake wawili. Jaymah Hapa ametesa na baadhi ya vibao vyake ni pamoja na Milele na Ulinitega. Msanii huyu anajaribu kuelezea safari yake ya Mapenzi katika wimbo wake wa “Ulinitega” alimthamini na kumwamini binti ya mtu akamtunuku Mtima wake zawadi aliyopata ni kutelekezwa na binti huyo kisha akaenda na Rafiki wake wa karibu. Nilizungumza Nae na akanielezea kuwa haamini iwapo mapenzi ya dhati yapo. Dah!

Bendi Hii ilianzishwa mwaka mmoja uliopita na chini ya miezi miwili wameweza kuachia nyimbo tatu. Nazo ni Bado(Afropop fusion),,BALAA ambayo imeweza kuwasongesha hatua kubwa. Wimbo huu uliwawezesha kufanya Mahojiano yao ya kwanza katika Radio Citizen (Mambo mseto) na Citizen TV (Mseto East Africa). Hivi sasa kundi hili limeziteka anga za muziki nchini na wimbo wao Mpya Hisia.
Watatu hao wanalenga kuwa kundi bora nchini chini ya mwaka mmoja na wanaamini kuwa miaka ijayo mitatu watakuwa kundi la kutazamwa na kupigiwa Mifano Afrika. Unaweza kuwafuata Mitandaoni

@SKY254 kisha utazame Nyimbo zao YouTube

About the author

Pizzah Mwitu

Pizzah Mwitu

A poet,,script writer,,a model,designer,,an actor,, an inspirational artist who believes he will one day change the world

Leave a Comment