Relationship

Tatu Wangu

Ken Kibet
Written by Ken Kibet
Spread the love

Alikua mtoto wa mwisho na wa kutajika kwa kila hali.
Mtaani walimwita Dida, mie nilimwita Tatu, aliitwa Amina Dida Tatu. Alizaliwa mnamo tarehe sita mwezi wa tisa mwisho ya hiyo karne enzi za babu. Alikua mtoto wa mwisho na wa pekee wa mzee mwite. Ni kweli Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo na Tatu alikua mpini wa ustaarabu. Tulikua wandani na marafiki wa karibu, Tatu alipenda kuwa msaidizi kulipotokea taabu, tukizisukuma wiki, nilianza kumwita Tatu wangu. Nakumbuka vyema alivyopenda kuwa mama, na mimi baba enzi za cha baba na cha mama. Tatu alikua mtulivu darasani, mnyamavu mikutanoni, Tatu alizifuata sheria zote bila maswali, alikua na bidii za mfanyikazi na hali hiyo ilimfanya wa kuigwa. Kidole kizuri huvishwa na nakumbuka akipewa zawadi ya kuongoza mtihani wa mkoa na hivyo alijulikana mjini na hata vijijini. Baada ya mda usiokua mrefu, Tatu wangu alimaliza masomo yake na kupata kazi kama *……..* kortini. Wakati huu wote mie na Tatu wangu bado tulikua marafiki hadi watu wakaanza kuniuliza lini ntaenda kwa goti na kumwitisha uhali. Wakati huo, bado nilikua natafuta kazi nikizunguka hapa na pale angalau kuunda riziki. Siku ilifika na hatimaye nikaamua kumjulisha Tatu wangu hali ilivyo nikitarajia angalau jibu halisi. Ningependa sana kuwa nawe,lakini natafuta mwanaume atakaye nienzi na kuniweka ninavyo stahili ndio yalikua majibu yake. Kwa masikitiko nilimwondokea na kumtazama tu kwa umbali. Alipohitimu umri, alipatana na kizee tajiri aliyemwaga pesa kama jasho, akamwoa, Akamtunza, na hata wakabarikiwa na mwana. Mwalimu Musa, ambalo ilikua jina la mlinzi wa Tatu wangu sasa, alimpenda Tatu kwa dhati naye Tatu alimpenda si haba na japo hali hiyo iliniumiza, ni kweli wawili hawa walipendana kama chanda na Pete,kama meno na gamu,kama mate na ulimi.
Ungewaona ungedhani ni siku yao ya harusi ila ilikua kila siku tu. Baada ya miezi sita, tisa hivi, hali ilianza kubadilika na Mwalimu Musa akawa si wa kusemeka tena. Musa akawa harudi nyumbani, akawa hamskizi Tatu chumbani,akawa anamnyima Tatu ruhusa ya kuenda mikutanoni, kila Tatu alijaribu kumuuliza mumeo ni yepi yaliomwingia,Musa alimgeuza mitungi. Tatu alijaribu kulivumilia hili jitu lakini iliyo na mwanzo kina mwisho na mwisho wa safari hili lilikua tayari limefikiwa na Tatu akafunga virago na kutorokea mjini nyeri alikopatana na mwarabu mstaarabu aliye lipia uuguzi wa majeraha yake na hata akampa hela ya kuanzisha biashara ndogo ili aweze kumlisha na kumtunza mwanao. Amini usiamini, nilipokua mjini nyeri raundi zangu za kila siku, nilipatana naye Tatu wangu akiuzauza njugu kwa madirisha ya magari ili kumlisha na kumtunza mwanao. Aliponiona, alinikimbilia na kunikumbatia kwa nguvu huku machozi yakimtiririka ila sikujua kama yalikua ya furaha au huzuni. Ni kweli maisha yalikua yamemwendea mrama Tatu Wangu. Ila nina swali, ni nani kati yenu, katika hii karne, ana uwezo wa kuinua mkono na kumpiga mkeo au mumeo? Na ni nani kati yenu wanaume anahaki ya kutozwa msichana mrembo na wa pekee, kumvunja ubikra, kumtaja Mungu kwa ritari ukimvisha pete kwa jina la baba, na la mwana na la roho mtakatifu, kisha kumgeuza mitungi??
Kenny,
Tatu wangu,
shairi maksudi.

About the author

Ken Kibet

Ken Kibet

Email: kenkibet254@gmail.com
Tel: +254708583561
IG: Poet Kenny.
Fb: Kemboi Kibet.

Spoken word artist. Call/text for event booking.

Leave a Comment