Lifestyle

UMAARUFU WAO NI NINI?

Spread the love

Je unawafahamu?
wengi wanawatambua kama Derah na Octo.umaarufu wao umewafanya wengi kuuliza vijana hawa ni kina nani na wanafanya nini? Usiulize tena.
Derrick Derah na Nick October (Octo) ni wanafunzi wa mwaka wa pili katika chuo kikuu cha Jaramogi Oginga Odinga.wote wana wanafanya shahada chini ya kitivu cha hisabati wakisomea Utakwimu Bima (Actuarial Science).
Wawili hawa wamekua maarufu sana chuoni hasa baada ya kuzindua biashara kubwa ambayo haijawapa Jina tu bali pia imewawezesha kujiendeleza pakubwa maishani hasa maisha ya chuoni.
Derah ambaye anafurahia kusafiri, kupiga soga na wenzake na kutizama filamu mfululizo(series) anashrikiana na Octo ambaye anafurahia kusafiri,kushiriki mashindano ya baiskeli na matembezi huru.wawili hawa wamekuwa ndugu Wa toka nitoke na urafiki wao hasa ndio chanzo chao kikubwa cha biashara ya vifurushi vya data.(bundles).
Katika kuwahoji Derah na Octo walisema kuwa waliianza biashara yao wakiwa katika mwaka Wa kwanza.wanasema kuwa walianza biashara hiyo Kwa kuuza filamu katika vyumba vya wanafunzi wenzao chuoni kama njia moja ya kujipa vijisenti vidogo Kwa ajili ya matumizi madogo madogo pale chuoni.Biashara hiyo haikuwa maruufu sana na hivyo basi wakaamua kujaribu biashara ya vifurushi data yaani bundles na nyota yao ya jaha iling’aa pale ambapo biashara hio ilipiku biashara nyingi pale chuoni na kunawiri haraka kutokana na idadi kubwa ya wateja.hali ya utata hasa katika “Wi-Fi” pale chuoni na vilevile wingi Wa kazi uliohitaji utafiti mwingi kwenye mtandao Wa Google iliwaletea wateja wengi.Wawili hawa wamekuwa wakiendeleza biashara yao Kwa muda mrefu hasa ikisemekana kuwa bei yao ni nafuu na inayokubaliwa na wanafunzi chuoni.

biashara hii ya uuzaji vifurushi vya data sasa imepata jina maalum hasa vyuoni kama “vifurushi mwitu” na Inapendwa sio na wanafunzi tu Bali pia baadhi ya wahadhiri hutumia vifurushi hivi.ni biashara ya kufana sana kwani Derah na Octo watakueleza kuwa biashara hii imewawezesha kufaulu katika mambo mengi.kwanza wanasema kuwa biashara hii imewawezesha kujikimu pale chuoni na kurahisisha majukumu na mahitaji mengi ya chuo yanayohitaji pesa.vilevile wawili hawa wameweza kufungua duka la bidhaa pamoja na duka LA M-Pesa nje ya chuo chao.wanasema kuwa biashara hii imewapa umaarafu sana hasa miongoni mwa vijana ambao wamewapa pongezi Kwa kazi yao.
hata hivyo wawili hawa wanasema kuwa wamekutana na changamoto kadhaa katika kazi yao.Mara nyingine hufedheheshwa na wateja ambao huchukua vifurushi vile na kukosa kulipia huku wakitoa vijisababu na hata kutoenakana tena.wakati mwingine hupoteza wateja wengi hasa kazi za darasa zinapokuwa mingi zaidi na pia wakati mwingine kiwango cha wavu (network) huwa chini zaidi na hivyo kuchelewesha kazi yao.

Kando na Dera na Octo kufanya biashara hii ya vifurushi,wawili hawa ni wanamitindo na wapangaji Wa events sherehe au matukio mbalimbali.
wao ni washiriki na wahusika wakuu wa kikundi maarufu kijulikanacho kama “Trap Nation Media” na wamefaulu katika kupanga na kumleta mwanavyombo wa muziki (DJ) Kalonje kwenye kilabu cha ‘Sponsers Lounge’ .

wana mipango maalum ikiwemo kufanikisha maonyesho ya wanamitindo(fashion Show) inayitarajiwa hivi karibuni.

wanasema kuwa wamejifunza mengi katika biashara pamoja na misafara ya ‘Trap Nation Midea’ kwani wameweza kukutana na watu Wa aina aina na kupata rafiki wapya ambao wameweza kuwasaidia sana katika maisha yao ya kila siku.
Sio siri kuwa wawili hawa wanahitaji nidhamu ya juu ili kukabiliana na changamoto za kazi wanazozifanya.wanasema kuwa nidhamu ya mtu binafsi ni muhimu mno kwani umaarufu huenda ukatibuka iwapo hutatii na kuiheshimu kazi unayoifanya.
ni vijana barobaro wenye
matumaini maishani na wameweza kuwa kielelezo Kwa vijana wengi Wa rika lao.Lengo lao kuu ni kutimiza ndoto zao maishani na kuwa mfano mwema Kwa kizazi cha Kesho.Jarida la Kampozone linatambua jitihada zao na Kuwapa pongezi Kwa kazi nzuri.
una maoni? una habari ambayo ungependa ichapishwe?Tuma ujumbe kwa wahariri @KAMPOZONE MAGAZINE.com

About the author

Gracey Eunice

Gracey Eunice

graceyeunice@gmail.com
Find what you love and let it kill you.
If my words ain't shit,neither am I.

Leave a Comment