Entertainment love Relationship

UTAMU WA BUSU.

Gracey Eunice
Written by Gracey Eunice
Spread the love

UTAMU WA BUSU.

Busu si busu tu, bali busu hukuambia mengi kuhusu mpenzi wako.Wanasayansi wamechunguza na kuhakikisha manufaa chungu nzima ya busu kwa binadamu.
Baadhi ya watu husema kuwa unapompiga busu mtu kisha uhisi kana kwamba umeme unapita mwilini mwako basi huyo anafaa kuoa/au kuolewa naye.
Wengine wankubali kuwa ukimbusu mtu na husikii raha hata kidogo basi hakufai.Wengine wanasema kuwa ufundi wa kupiga busu si kitu, muhimu ni wewe unavyojisikia baada ya busu.
Hata hivyo utamu wa busu hutegemea jinsi unavyolipiga busu hilo.Kwanza,ni muhimu kuwa unapopiga busu uyafunge macho.wewe pamoja na unayeshiriki busu mnapaswa kuyafunga macho yenu,hii ni kwa sababu :
1. Hutaki kujiona ulivyo wakati wa kupiga busu hasa la kifrench, vivyo hivyo mwenzi wako;
2. Ubongo hauwezi ku-zungusha ulimi wakati huo huo kupepesa macho….yaani kama vile kusema…Mpaka, Mkata, Msata haraka haraka..ubongo wako hauwezi kuyafanya hayo yote kwa wakati mmoja.
3. Ni vigumu (ufanisi hafifu)kubusu ukiwa macho wazi na pia ni ajabu kutoa miguno ya busu macho wazi;
4. Mfumo wa macho hautaki kuangalia kitu kwa ukaribu kiasi hicho;
5. Kwa wanawake, kufungua macho kunakuharibia utaratibu mzima wa kuvuta taswira mfano unaweza kufikiria kuwa una-mbusu Alejandro wakati aliye mbele yako ni Wasike.
6. Kwa Wanaume, kama unabusu baada ya kupiga raundi kadhaa Kipindi kizima kiangalau inakuwa rahisi kufikiria mambo mengine kama mpira n.k. ukiwa umefumba macho;
7. Ukiwa macho wazi pua ya mpenzi wako inaonekana kubwa kama Pua ya Lori-basi na hivyo kupoteza utamu wa busu.

Kuna aina tofauti za kubusu ili kutuma ujumbe kwa mpenzi wako na hasa kuupata na kuuhisi uhondo na utamu wa busu.
Unaweza ukapewa busu wewe ukadhani ni kawaida (kama hujui) lakini mwenzio anakwambia amechoka, anakupenda, anashukuru, amefurahi kukuona, hataki kungonoana siku/wakati huo, hana raha/hujamfurahisha, anataka kuwa peke yake, anamachungu, yuko busy n.k.Hivyo basi ili kufurahia utamu wa busu yafaa uwe makini wakati unapombusu mwenzi wako.

Ili mfurahie busu mnatakiwa kupeana (umbusu-akubusu) .
Jambo muhimu la kuzingatia ni kutokukusanya midomo yako kana kwamba unataka kubusu kwa sauti na badala yake busu kimahaba…..Hivyo basi,ili kuhisi utamu wa busu:

1.Sogeza midomo yako kama ilivyo (umeifumba lakini imelegea) kwenye midomo ya unayetaka kumbusu…..kisha itulize midomo hiyo juu yake na uweke“busu kavu” juu ya midomo yake kisha jitoe alafu rudi tena x3
2.Inua uso wake kwa kutumia kidole (hii ni kwa wanaume) na mbusu moja kwa moja kwa kugusanisha pua kiaina…-Busu kwa kupindisha shingo/kichwa ili kutogusanisha pua zenu…
3) Ukiwa umepindisha kichwa/shingo…mshike mkono au mkumbatie kiasi na busu tena.
Ukiona/hisi anajisogeza au anakupa ishara kuwa uendelee kwa kufungua mdomo kiaina, kukushika mkono/kifua/kitambi/kiuno au kuweka mkono kwenye bega basi endelea na “busu nyevu” kwa kubusu katika mtindo wa kulamba-kunyonya mdomo(lips) wa chini na tulia hapo kwa sekunde chache kisha pokea ulimi wake kwa ulimi wako (bila kuachama…ni mumo kwa mumo)alafu ukwepe na kisha rudi kwenye midomo ya juu…..
Ongeza ujuzi wako sasa…na kumbuka kupumua kwa kutumia pua sio unampumulia mwenzio mdomoni….(atashiba hewa) au unabada pumzi (Mauti inakukumba). Fumba macho na fikra zako uzitie kwa yule unayembusu.

Watu wengi hubusu tu kwa ajili ya kuonyesha wenzi wao kuwa wanajua tendon hilo ilhali ni wachache tu wanaohisi na kufurahia utamu wa busu.
Je,Siri umeipata?

About the author

Gracey Eunice

Gracey Eunice

graceyeunice@gmail.com
Find what you love and let it kill you.
If my words ain't shit,neither am I.

Leave a Comment